HabariKimataifa

UFARANSA YAHITIMISHA OPARESHENI YAKE YA UOKOAJI AFGHANSTAN…………

Ufaransa imehitimisha operesheni yake ya uokozi nchini Afghanistan.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Frorence Parly ameandika zoezi hilo limehitimishwa hapo jana jioni.

Amesema katika kipindi cha wiki mbili tu, jeshi la Ufaransa limefanikiwa kuwaokoa watu 3,000, wakiwemo Waafghan 2,600 ambao wameomba hifadhi nchini Ufaransa.Marekani itahitimisha zoezi hilo juma lijalo wakati hali ya kiusalama ikionekana kuzorota mjini Kabul. Ujerumani na Canada ni miongomi mwa mataifa ambayo yamehitimisha Alhamis, wakati Uhispania jana Ijumaa huku Uingereza ikufuata mkondo huo leo hii.