Naibu wa rais Dkt William Ruto amezuru maeneo ya mlima Kenya katika ziara yake ya kutafuta umaarufu eneo hilo uchaguzi mkuu wa mwaka ujao unapokaribia.
Akihutubia wananchi wa eneo bunge la Kieni Kaunti ya Nyeri, Ruto amewahakikishia wakaazi hao kwamba mipango yake na rais Uhuru Kenyatta ya kujenga mabwawa mawili ya maji ambayo yataghatimu takriban shilingi billioni 20 ili kutataua tatizo la maji eneo hilo atahakikisha kwamba mipango hiyo imeafikiwa.
Aidha, licha ya majaribio ya kumzuia kuzuru eneo hilo la kieni, Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa hatayumbishwa kwenye azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao na kwamba bado ataendelea kuzungumzia juhudi zake za kufufua uchumi wa nchi.
BY NEWS DESK