HabariNewsSiasa

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi amekanusha kujiunga na chama cha Democratic Party…

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi amekanusha kujiunga na chama cha Democratic Party na kutaja habari hizo kama uvumi huku akisisitiza kuwa bado hajaunda chama atakachotumia kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Akihutubia viongozi wa kidini Muturi amefafanua kwamba anataka kuwa rais ili ahakikishe maendeleo yanasambazwa kwa usawa katika sehemu zote nchini haswa eneo la Mlima Kenya Mashariki kwani anahisi kuwa eneo hilo limetengwa zaidi kimaendeleo nchini.

Wakati huohuo, Spika Muturi ametoa wito kwa viongozi wa kidini kumakinika zaidi na kuwatathmini viongozi wa kisiasa wanaogombea nyadhifa mbalimbali za uongozi  kwani viongozi wa kidini huchangia nafasi muhimu katika siasa nchni.

BY NEWS DESK