HabariSiasa

Rais atoa msaada wa mabasi kumi kwa shule za upili…..

Rais Uhuru Kenyatta ametoa msaada wa mabasi 10 kwa shule mbali mbali za upili na taasisi za kijamii humu nchini.

Miongoni mwa makundi yaliyonufainika ni muungano wa wa wanawake wa kanisa katoliki diosisi ya maralal na klabu ya marafiki ya football katika kaunti ya Nyeri.

Shule zilizonufaika na mpango huo ni ile ya wasichana wasiokuwa na uwezo wa kusikia ya Tumtum, shule ya upili ya marifano ya Tanariver, Achiengo girls Kisumu na oleruki school of Narok.

Nyingine ni shule ya upili ya Rukanga Kirinyaga, shule ya upili ya Mnegei Pokot Magharibi, miongoni mwa nyingine.

Rais Kenyatta pia ametoa msaada ya maski 2000 kwa shule za upili.

 

By reporter