HabariNewsSiasa

Mkurungenzi wa idara ya upelelezi wa jinai nchini ameanzisha uchunguzi .

Mkurungenzi wa idara ya upelelezi wa jinai nchini Gorge Kinoti ameanzisha uchunguzi kuhusiana na kutekwa nyara kwa mchanganuzi mmoja wa maswala ya kiafrika katika jiji la Nairobi.

Akizungumza na viongozi wa baraza la muungano wa kiislamu nchini ambao walijitokeza katika idara hiyo wakiitaka idara hiyo kuingilia kati swala la watu kupotea, Kinoti ameapa kuwa uchunguzi huo utafanyika ili wabaini alipo mchanganuzi huyo kwa jina Abdiwahab Sheik Abdisamad.

Aidha kulingana na bawabu mmoja aliyeshuhudia kisa hicho waliomteka nyara Abdisamad  walikuwa ni wanaume 4,mmoja ambaye alikuwa ana pingu huku mwengine akiiwa na bunduki.

BY NEWS DESK.