AfyaHabariNews

Madaktari kaunti ya Mombasa waanza mgomo rasmi hii leo….

Muungano wa madaktari KMPDU kaunti ya Mombasa  wametangaza kujiunga na mgomo wa wauguzi ambao umeingia wiki ya pili sasa.

Madaktari hao kutoka hospitali za umma kaunti hii ya Mombasa wameapa kuendelea kususia kazi kwani kwa muda wa miezi 3 sasa bado hawajalipwa mishahara yao.

kulingana  na katibu katika  muungano wa madaktari katika ukanda huu wa pwani Dkt Nasir Shaban,  kufikia sasa kuna madaktari ambao hawajapata bima yao ya afya na madaktari hao wanafanya kazi katika kitengo cha kuwauguza wagonjwa wa virusi vya korona.

Aidha kwa sasa wagonjwa walioko katika kaunti ya Mombasa wameshauriwa kutafuta huduma za afya katika hospitali nyingine ikiwemo ile ya rufaa ya msabweni,Mariakani pamoja na Kilifi.

Madaktari hao wameafikia hatua hiyo baada ya juhudi zao kuwasiliana na usimamizi wa serikali ya kaunti kugonga mwamba.

BY NEWS DESK