HabariNews

Watoto wawili wafariki papo hapo baada ya kushambuliwa na fisi huko Kinango….

Watoto wawili wa kati ya mwaka 1 na 2 wamefariki papo hapo huku watu 3 wakiachwa na majeraha baada ya kushambuliwa na fisi (hyena) katika kijiji cha Baisa huko kinango kaunti ya Kwale.

Ocpd eneo la kinango Fredrick Ombaka amethibitisha tukio hilo akisema kwamba fisi huyo amewapasua vichwa watoto hao Lugo Nyale wa miaka 2 na mwenzake Mbodze Nyawa wa mwaka 1 kisha kula ubongo wao kabla ya mama ya mmoja ya mwendazake Mbodze Nyawa anayefahamika kwa jina Mulongo Tsimba kupiga kamsa zilizowavutia wanakijiji waliomshambulia fisi huyo ambaye kabla ya kuuwawa aliwaacha watatu hao na majeraha.

Waliojehuriwa wamekimbizwa katika hospitali ya samburu kwa matibabu huku miili ya wendazake ikihifadhiwa katika mochari ya hospitali ya kinango ikisubiri upasuaji.

Mizoga wa fisi huyo ukichukuliwa na maafisa wa kws kwa uchunguzi zaidi

Haya yanajiri huku taharuki ikitanda katika kijiji cha Wasaa kaunti ya Kwale kutokana na uwepo wa nyati ambaye anawahangaisha wenyeji.

Wakazi wa Kikoneni wanasema kwamba shughuli za ukulima eneo hilo zimeathirika pakubwa kwa sababu mara nyingi wanapolima mahindi nyati huyafanya kitoweo mazao yao ya shambani.

Aidha Mwanamume mmoja amevamiwa na kuvunjwa mguu na Nyati wakti akiwa malishoni.

Haya yanajiri licha ya serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium pamoja na idara ya wanyama kuendesa zaoezi ya kuwahamisha Nyati na ambapo walihamisha nyati tisa na kuwapeleka katika mbuga ya wanyamapori ya Tsavo kaunti ya Taita Taveta mwaka jana.

BY NEWS DESK