HabariKimataifaNews

Watu 13 watiwa mbaroni Rwanda wakituhumiwa kupanga mashambulio ya “kigaidi”

Polisi ya Rwanda imesema, imewatia mbaroni watu 13 wanaoshukiwa kupanga mashambulio ya “kigaidi” dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo Kigali na kuwaonyesha watuhumiwa hao kwa vyombo vya habari.

Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Taifa ya Rwanda imesema, watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vifaa kadhaa vya kutengeneza mabomu zikiwemo mada za miripuko, nyaya, misumari na simu za mkononi.

“Uchunguzi umeonyesha kuwa kikundi hicho cha kigaidi kilikuwa kikifanya kazi kwa kushirikiana na Vikosi vya Muungano wa Kidemokrasia (ADF)”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya Polisi ya Rwanda ikimaanisha kundi hilo la kigaidi linaloendesha harakati zake mashariki mwa nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

BY NEWS DESK