HabariNews

Wito watolewa kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kama wapiga kura .

Wito umetolewa wa wakaazi eneo bunge la Malindi kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kama wapiga kura ili waweze kuwachagua viongozi watakao leta mabadiliko eneo hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanasiasa Philip Charo amesema kupitia uchaguzi wakaazi watamaliza masaibu wanayopitia kwa sasa.

Amesema njia pekee ya kuhakikishia wakaazi maendeleo ni kupitia kushiriki uchaguzi kutumia kadi za kura.

Wakati uohuo Charo amewashauri maafisa wa idara ya vitambulisho kuharakisha zoezi la utiaji wa vitambulisho ili waweze kupata kadi za kura.

Amewarai wakaazi kufika vituoni mapema badala ya kusubiri hadi dakika za lala salama za zoezi hilo.

Kauli ya mwanasiasa huyo inajiri huku zoezi hilo la kuwasajili wapiga kura wapya likitazamiwa kuanza rasmi siku ya jumatatu.

BY NEWS DESK