AfyaHabariNews

Hatuna uwezo wa kulipa bima ya NHIF wasema wananchi wa kawaida.

Hisia mseto zimeibuka miongoni mwa wakenya baada ya mswada kuhusu Bima ya afya kupitishwa hapo juzi.

Mswada huo uliopitishwa na wabunge umehimiza kuwa ni lazima  kila mwananchi kulipa shilingi 500 ya Bima ya Afya kila mwezi.

Katika mtaa wa Utange eneo bunge la kisauni  muakilishi wa nyumba kumi Mama Fatma ameitaja hatua hiyo kama ya kumkandamiza mwananchi wa chini kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Aidha ameitaka serikali kuujadili upya mswada huo.

BY NEWS DESK