HabariNews

Waziri wa Elimu George Magoha aumiminia sifa mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Waziri wa Elimu George Magoha ameumiminia sifa mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Akiongea katika warsha ya uzinduzi wa chuo cha ufundi cha Nyandarua katika kaunti ya Nyandarua, Waziri amesema mtaala huo utawapa wanafunzi maarifa tofauti tofauti na iwe rahisi kwao kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa.

Aidha ameukashif mtaala wa 844 kwa kudai kuwa ulikua ukiwapa wanafunzi maarifa ya kitabu tuu na kuwafanya wategemee zaidi kuajiriwa kuliko kujiajiri.

Kwa upande mwengine Magoha amewataka wanafunzi kutoka kaunti ya Nyandarua kujiunga na Chuo hicho na kuboresha uvumbuzi kwenye kilimo ili kupunguza gharama ya kuingiza vitu kutoka nje.

BY NEWS DESK