HabariNews

SIKU YA WALIMU DUNIANI YAADHIMISHWA HII LEO.

Hii leo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya walimu Duniani, Shirika la Kitaifa la ubunifu KNIA limetoa pendekezo kwa wizara ya Elimu kufadhili kikamilifu mipango yakuwafundisha walimu kuhusu mtaala wa umilisi CBC.

Mwenyekiti wa Shirika hilo  Professor Roban Maruwanga ameishauri Serikali kudhihirisha uimara wa CBC kwa kufadhili masomo yote ya Walimu.

Maruwanga amesema kwamba idadi kubwa ya shule za Umma humu Nchini hazina vifaa vya kutosha kama vile madarasa na maabara hali ambayo inatishia utekelezaji wa mtaala ho mpya.

Kwa mujibu wa Profesa Maruwanga, mabadiliko mengi katika sekta ya Elimu yanahitaji ufadhili mkubwa kutoka kwa Serikali ili kukabili changamoto zinazoibuka.

Profesa Maruwanga ameikosoa hatua ya Serikali kuwataka walimu huku wakiwemo wanaopata mshahara wa shilingi elfu 20 pekee kutoa shilingi elfu sita kila mwaka ili kujifundisha kuhusu mtaala wa CBC akikariri kwamba mtaala mpya haufai kuwa mzigo kwa wazazi wala walimu.

BY NEWS DESK