HabariNews

WAKILI TAJIKA KWA JINA EVANS MONARI AAGA DUNIA.

Wakili tajika ambaye pia amekuwa akiugua kwa mda mrefu kwa jina Evans Monari ameaga dunia.

Wakili Monari amekuwa akiugua kwa mda na kulazwa katika Hospitali ya Nairobi kwa takriban mwezi mmoja uliopita akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha ICU.

Kwa wakati mmoja wandani wake waliomba usaidizi kugharamia matibabu yake baada dawa za matibabu kufikia shilingi milioni 16 na kampuni ya Bima kukataa kushughulikia dawa hizo.

Wakili Monari alipata umaarufu baada kwa kumwakilisha Rais Uhuru Kenyatta katika Mahakama ya ICC  na katika kesi nyengine kadhaa akiwa miongoni mwa Wakili  wengine.

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha wakili Evans Monari aliye aga dunia alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi.

Rais Uhuru amemtaja Wakili Monari kuwa miongoni mwa wakili aliyejipatia sifa kwa weledi wake miongoni mwao.

Mbali na Rais Uhuru Kenyatta, Wakili Monari ameombolezwa na mawakili wengi humu Nchini ambao walifanya kazi naye na vile vile wale waliomtambua kwa uwezo wake kazini.

BY NEWS DESK