HabariNews

Naibu Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani hii leo ametoa hundi za bursary zenye thamani ya shilingi milioni 1.2….

Naibu Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani hii leo ametoa hundi za bursary zenye thamani ya shilingi milioni 1.2 chini ya mpango wa elimu ni sasa kwa wanafunzi 98 wa vyuo vikuu, vyuo vya anwai, shule za upili pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kiufundi katika wadi ya Vanga, gatuzi dogo la Lunga Lunga.

Kwenye hotuba yake, Achani amesema kuwa kaunti ya Kwale imepiga hatua muhimu katika sekta ya elimu.

Achani ameongeza kwamba mpango wa Elimu ni sasa umeunda jukwaa la kuwasaidia  wanafunzi wa Kwale kupata elimu katika taasisi mbalimbali.

Kaunti ya Kwale inajivunia kuwafadhili zaidi ya wanafunzi 5000 katika shule za upili za kitaifa, zaidi ya wanafunzi 3500 katika vyuo vikuu na wanafunzi 55,000 katika vyuo vya ufundi.

BY NEWS DESK