HabariNews

WAKAAZI WA TIWI ENEO BUNGE LA MATUGA KAUNTI YA KWALE WAANDAMANA.

Wakaazi wa Tiwi katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale wameandamana kulalamikia unyakuzi wa mashamba yao na mabwenyenye.

Wakiongozwa na Hamisi Mwajawa, wakaazi hao wamedai kwamba mabwenyenye hao wamekuwa wakivamia mashamba yao tangu yapimwe na serikali mwaka wa 1972.

Ni hali ambayo imezipelekea zaidi ya familia elfu moja kuishi kama maskwota baada ya kuathirika na mzozo wa umiliki wa ardhi ya ekari 960 katika eneo hilo.

Wakaazi hao wanaodai kwamba wamiliki wa ardhi hiyo sasa wanamtaka waziri wa ardhi nchini Farida Karoney kuingilia kati ili kutatua mzozo huo.

Aidha, wenyeji hao wameitaka serikali kupitia tume ya kitaifa ya ardhi (NLC) kupima upya ardhi zao na kuwapatia stakabadhi za umiliki.

BY NEWS DESK