HabariNewsSiasa

Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi ahaidi kushughulikiwa suala la uhaba wa maji iwapo atakuwa gavana.

Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi na ambaye pia anakimezea mate kiti cha ugavana kaunti hiyo amesema kwamba iwapo atafanikiwa kuwa gavana wa kaunti ya Kilifi atahakikisha swala la uhaba wa maji linashughulikiwa vilivyo.
Akizungumza na Sauti ya Pwani Fm katika kipindi Baraza Letu Kahindi amesema kwamba atahakikisha kuwa sheria waliopitisha mwaka wa 2014 ya water and sanitation services inayolazimu serikali ya kaunti kutumia rasilimali za kaunti ili kuhakikisha wananchi na mifugo yao wanapamata maji safi na huduma nzuri, inatimilizwa kikamilifu.
Wakti huo huo akizungumzia swala la jinsi atahimarisha elimu kaunti ya Kilifi ili kupunguza visa vya mimba za mapema, Kahindi ameahidi kwamba atahakikisha wanapeana ufadhili kwa wanafunzi kwa asilimia 100 kinyume na mpango wa utoaji basari ambapo wanafunzi wengine hukosa.
Hata hivyo amedokeza kwamba serikali ya Kilifi hutenga takriban shilingi milioni 350 kila mwaka ili kuwasaidia wanafunzi kuenda shule.

By Joyce Mwendwa