Muungano wa madaktari nchini KMPDU unapanga kufanya mgomo wa kitaifa wakishtumu serikali za kaunti kwa kupuuza kutekeleza matakwa ya madaktari hao.
Wakizungumza hapa Mombasa kwenye kongamano la 7 la kila mwaka lililowaleta pamoja wajumbe wa muungano huo, muungano huo umedokeza kwamba tume ya kushughulikia mishahara SRC imewapunguzia marupurupu yao huku wakisistiza kwamba kuna haja ya kuwepo kwa mkataba wa pamoja wa maelewano CBA katika kila kaunti.
Muungano huo aidha umeitaka serikali kuweka fedha zaidi kwenye sekta ya afya za kununua madawa na vifaa vitakavyo tumiwa na madaktari pamoja na kuangazia janga la corona.
By Nick Waita