HabariNewsSiasa

NAIBU WA RAIS WILLIAM RUTO ARINDIMA SIASA ZA BOTTOM UP.

Naibu wa Rais William Ruto amewasili katika eneo la Kasemeini, Kibwezi Magharibi ambapo amekutana na zaidi ya wajumbe 1000 wa eneo la Ukambani wa Chama chake cha UDA.

Ruto amelakiwa na Mshirikishi wa Chama cha UDA eneo la Makueni James Mbaluka ambaye ameandamana na wabunge Ndindi Nyoro wa Kiharu, Victor Munyaka wa Machakos Mjini, Gavana wa Turkana Joseph Nanok na aliyekuwa Gavana wa Machakos Johnson Muthama ambaye ndiye Mwenyekiti wa UDA.

Wakati uo huo ameendelea kupigia debe miradi ya Serikali iliyoanzishwa na kufanikishwa katika Kaunti ya Makueni huku akitaja miradi kadhaa ya Barabara ambayo na inaendelezwa akisema kwamba ni ishara ya maendeleo mengi zaidi ambayo anaweza kutekeleza iwapo atateuliwa kuwa Rais.

BY NEWS DESK