HabariNewsSiasa

JAJI MKUU MARTHA KOOME ASHINIKIZWA KUAPISHWA KWA MAJAJI SITA.

Jaji Mkuu Martha Koome ameshinikizwa kuapishwa kwa majaji sita waliokuwa wameachwa na Rais Uhuru Kenyatta alipowateua wengine 34.

Kwenye mahojiano na Rais wa Chama cha Wanashreia humu Nchini LSK Nelson Havi, amemtaka kutii agizo la Mahakama kwamba Jaji Mkuu atakuwa huru na anaweza kuapisha baada ya siku 14 kukamilika pasi na Rais kuapisha.

Itakumbukwa kwamba mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Kihara tayari amekata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa wiki iliyopita.

BY NEWS DESK