HabariNewsSiasa

Vijana wana imani ndogo na tume ya uchaguzi ya IEBC asema Edwin Sifuna.

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amesema kwamba idadi ndogo inayoshuhudiwa ya vijana wanaojitokeza kusajiliwa kama wapiga kura, imetokana na vijana kuwa na imani ndogo na tume ya uchaguzi ya IEBC.

Kulingana na Sifuna ni kwamba vijana wanahisi kuwa huenda kura zao zisichangie pakubwa katika uchaguzi mkuu ujao, hivyo basi kuitaka IEBC kushughulikia swala la wakenya kutokuwa na imani nao.

Kwa upande wake aliyekuwa naibu mwenyekiti wa IEBC Mahiri Zaja amesema kuwa takriban watu milioni 4.6 wangali bado hawajasajiliwa hivyo basi IEBC haina budi ila kutii uamuzi huo ili kuafikia lengo la kuwasajili wapiga kura wapya milioni 6.

Zaja vilevile ameitaka IEBC kutafuta fedha zaidi kutoka kwa wizara ya fedha ili kufanikisha zoezi hilo.

BY JOYCE MWENDWA