HabariNews

Maseneta wamtaka waziri wa elimu prof George Magoha pamoja na wakuu wa chama cha shule za upili KESHA kufika mbele yao.

Maseneta wamemtaka waziri wa elimu George Magoha pamoja na wakuu wa chama cha shule za upili KESHA kufika mbele yake kutoa maelezo kuhusiana na kukithiri kwa visa vya uteketezaji wa majengo ya shule.

Maseneta hao aidha wamelalamikia utovu wa nidhamu ya wanafunzi miongoni mwa wanafunzi vilevile kipindi kirefu cha masomo ili kufidia muda uliopotezwa wakti shule zilikuwa zimefungwa kutokana na janga la Corona kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kwa ongezeko la uteketezaji wa majengo shuleni.

Haya yanajiri huku shule ya wavulana ya Chavakali ilioko kaunti ya Vihiga ikifungwa hii leo kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana na kuharibu mali shuleni humo.

BY NEWS DESK