HabariNewsSiasa

Ann Kananu Mwenda ameapishwa kuwa gavana wa tatu wa kaunti ya Nairobi.

Kananu ambaye amehudumu kama naibu gavana tangu mwezi disemba mwaka uliopita baada ya kung’atuliwa kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko, ni mwanamke wa wanne nchini kuchukua usukani kama gavana.

Ameongoza kwamba yupo tayari kushirikiana na viongozi wa jimbo hilo ili kuhakikisha kwamba sifa za jiji la Nairobi zinarudi kama ilivyokuwa awali na vilevile kuhakikisha wakaazi wa Nairobi wanapata huduma bora na za hali ya juu.

Kananu aidha amewahimiza wanawake kujitokeza na kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi.

Hafla hii ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi, imefanyika katika ukumbi wa KICC.

BY NEWS DESK