HabariNewsSiasa

Teddy Mwambire amewataka wafuasi wa chama cha ODM kuwa wavumilivu…

Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi na aliyepia mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa wavumilivu kutokana na hatua ya kinara wa chama hicho Raila Odinga kufeli kufungua ofisi ya makao makuu ya chama hicho.

Mwambire amesema Odinga anatarajiwa kuzuru tena kaunti ya Kilifi mwezi ujao kwa shughuli ya kuifungua rasmi ofisi hiyo pamoja na kuwapokea wanasiasa waliohamia ODM kutoka vyama vingine.

Aidha ameongeza kuwa shughuli hiyo iliyoratibiwa kufanyika hapo jana ilikosa kutekelezwa kufuatia kukosekana kwa muda kutokana na ratiba ya ziara ya Odinga kukatizwa ili kwenda kuomboleza pamoja na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff aliyepoteza wafanyakazi wanne kwa ajali ya barabarani.

Ikumbukwe kinara wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku tatu ukanda wa pwani hii leo kwa kuhudhuria mikutano kaunti za Mombasa na Kwale.

BY NEWS DESK