HabariNewsSiasa

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti ahukumiwa.

Mahakama kuu imemhukumu mkurugenzi wa idara ya upelelezi na jinai DCI George Kinoti kifungo cha miezi minne jela.

Akitoa uamuzi huo jaji Anthony Mrima ameagiza Kinoti azuiliwe katika gereza la Kamiti kwa kukiuka agizo la mahakama la kurudisha bunduki nyumbani kwa mfanyibiashara Jimmy Wanjigi.

Aidha Kinoti amepewa siku saba kujisalimisha na iwapo hata fanya hivyo inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ameagizwa kumkamata.

Mapema mwaka huu Kinoti alipewa siku 30 kurejesha bunduki za mfanyibiashara huyo kulingana na agizo lililotolewa mwaka 2019.

Hata hivyo makataa dhidi ya Kinoti yalikamilika tarehe 25 machi mwaka huu.

BY NEWS DESK