HabariNewsSiasa

Viongozi waasi wa chama cha ODM wasema ziara ya Raila Odinga mkoani pwani haikuwa na umaarufu.

Viongozi waasi wa chama cha ODM wamesema kuwa ziara ya Raila Odinga mkoani pwani haikuwa na umaarufu hii ni siku mbili tu baada ya kinara huyo kukamilisha ziara yake.

Viongozi hao chini ya naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Kilifi Sammy Ndago wamesema kuwa chama cha ODM hakina tena umaarufu ukanda wa pwani kwani hata baadhi ya viongozi ukanda wa pwani walisusia ziara hiyo.

Kulingana na viongozi hao ambao kwa sasa wanaegemea upande wa Pamoja African Alliance PAA ulio chini ya Gavana Amason Kingi ni sharti kinara huyo wa ODM atafakari upya msimamo wake na kufanya kazi na vyama vya ukanda wa pwani.

BY NEWS DESK