MombasaNewsTechnology

Wito watolelwa kwa vijna humu nchini kujihusisha na kazi za mitandaoni (Online Jobs).

Wito umetolelwa kwa vijna humu nchini hasa wale ambao hawana ajira katika maeneo mbalimbali kujihusisha kufanya kazi kupitia kwa mitandao.
Akizungumza kuhusu suala hilo, Katibu mwandamizi katika wizara ya habari na teknolojia Maureen Mbaka amesema kwamba, vijana wa nchi hii wanafaa kuchukua fursa ya mpango wa Ajira digital ambao ni mpango wa serikali unaotoa mafunzo kwa vijana ya kufanya kazi kwenye mtandao kupitia mfumo wa ajiradigital.go.ke.
Wakati uo huo, Mbaka aidha amesema kwamba serikali imebuni vituo vya shughuli za dijitali katika maeneo bunge nchini ambavyo pamoja na mpango wa Ajira digital, vimewezesha vijana milioni 1.2 kushiriki kwenye kazi ya mitandaoni.
Hata hivyo, mbaka amesema kwamba halmashauri ya teknolojia ya habari na mawasiliano iko mbioni kuendeleza usambazaji wa kebo za mawasiliano za fiber optic ili kuwezesha sehemu nyingi zaidi hapa nchini kuunganishwa na mitandao.