AfyaHabariKimataifaNewsWorld

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO LATAFUTA MKATABA MPYA WA KUKABILIANA NA KIRUSI KIPYA CHA OMICRON

Shirika la Afya Duniani WHO na washirikishi wengine inatafuta mkataba mpya wa kukabiliana na janga la kirusi kipya cha Omicron.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao maalum cha WHO, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom, amesema kwamba janga la Corona limeweka wazi udhaifu uliopo katika mfumo wa maandalizi na majibu ya majanga duniani huku akiongeza kwamba njia nzuri ya kukabiliana na majanga hayo ni kwa kupitia makubaliano ya kisheria kati ya mataifa, makubaliano yanayotokana na kutambua kwamba, hakuna hatma isipokuwa hatma ya pamoja.
Ingawa WHO imesema Kamba bado haina uwazi kama virusi vya Omicron vinaambukiza zaidi ama vina dalili kali zaidi kuliko virusi vya aina nyingine ikiwemo Delta, wasiwasi umeongezeka juu ya athari yake kwa chanjo za COVID-19 zilizopo kwa sasa pamoja na matibabu