AfyaHabariNews

WAZIRI WA AFYA MUTAHI KAGWE AITISHA MKUTANO WA DHARURA KUJADILI MBINU ZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameitisha mkutano wa dharura kujadili mbinu za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona msimu huu ambapo wakenya wanajiandaa kuanza msimu wa Krismasi.
Mkutano wa leo unatarajiwa kuhudhuriwa na washika dau wa sekta ya afya wakiwemo wenzao wa Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia majanga ambayo ilibuniwa Mwezi Februari Mwaka uliopita kuishauri Serikali kuhusu masuala ya Janga la Corona.
Mkutano huo unajiri siku mbili baada ya Katibu katika Wizara hiyo Susan Mochache kutangaza kwamba Serikali haina mipango yoyote ya kudhibiti safari za nje na Kaunti mbali mbali baada ya aina tofauti ya virusi vya Corona kuripotiwa kuzuka katika Taifa la Afrika Kusini.