HabariNews

FAHALI WAWILI JIMMY WANJIGI NA MKUU WA IDARA YA DCI GEORGE KINOTI KUKABILIANA KISHERIA MAHAKAMANI HII LEO.

Makabiliano ya kisheria yanatarajiwa Mahakamani baina ya Mfanyibiashara Jimmy Wanjigi na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Upelelezi DCI George Kinoti kufuatia ombi la kumtaka Kinoti kumkamata Wanjigi kwa kumiliki silaha nyingi.
Ombi hilo liliwasilishwa Mahakamni na Mkenya mmoja kwa Jina Membo Ocharo akidai kwamba hatua ya Wanjigi kumiliki silaha hizo inahatarisha usalama wa Kitaifa.
Kupitia Wakili wake Dastan Omar, Ocharo amedai kwamba iwapo agizo la Mahakama ka kutaka Wanjigi arejeshewe silaha zake litatekelezwa, basi huenda likawaweka Wakenya hatarini kutokana na Wanjigi kumiliki takriban ya silaha 700.