GamingHabariNewsSports

NICK MWENDWA AJIONDOA KATIKA WADHIFA WA RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA FKF.

Nick Mwendwa amejiondoa katika Wadhifa wa Rais wa Shirikisho la Soko humu Nchini FKF.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikiwa kamati kuu ya kitaifa ya FKF, Nick Mwendwa amesemwa kwamba majukumu yake sasa yatatekelezwa na Naibu wake Doriss Pethra kuambatana na kifungu cha 42 ibara ya 8 ya Katiba ya shirikisho hilo.
Akitoa sababu za kujiondoa kwake, Nick Mwendwa amesema kwamba amechoshwa na visa vya kukamatwa na maafisa wa polisi na kuzuiliwa kila mara, matukio ambayo anadai kwamba yameathiri pakubwa family na biashara zake.
Wakati uo huo Mwendwa ameeleza Imani na matumaini yake kwamba mwishowe ataachiliwa huru baada ya kutopatikana na hatia yoyote.
Barua hiyo imejiri saa chache tu baada ya Rais huyo kukanusha mashtaka ya uwizi wa shilingi milioni 38 za shirikisho hilo la FKF mbele ya Hakimu Mkuu wa Milimani Eunice Nyuto ambaye alimuachilia kwa dhamana ya shilingi milioni 10.
Mwendwa aidha ametakiwa kutozuru ofisi za FKF, kuwasiliana