HabariKimataifaNewsWorld

Watu wanne wameshtakiwa kwa kumchinja na kumchoma moto hadi kufa mzee mmoja nchini Msumbiji ambaye ametuhumiwa kuwa mchawi.

Watu wanne wameshtakiwa kwa kumchinja na kumchoma moto hadi kufa mzee mmoja nchini Msumbiji ambaye ametuhumiwa kuwa mchawi.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 73 ameuwawa huko Zavala kusini mwa mkoa wa Inhambane.
Tukio hilo limetokea baada ya mganga wa jadi kumshutumu mwanamume huyo kwa kuhusika na mauaji ya vijana wawili.
Mmoja wa wakuu wa Chama cha Madaktari wa Jadi wa Msumbiji, katika wilaya ya Zavala, pia amefunguliwa mashtaka kwa kosa la kuwaweka wazee hatarini.
Inaripotiwa kwamba wananchi walimpiga mzee huyo baada ya mganga huyo wa jadi kumhusisha na uchawi.