HabariMazingiraNews

Waziri wa Uchukuzi na ujenzi James Macharia amesema kwamba Kenya inakabiliwa na upungufu mkubwa wa nyumba.

Waziri wa Uchukuzi na ujenzi James Macharia amesema kwamba Kenya inakabiliwa na upungufu mkubwa wa nyumba, jambo ambalo linahitaji mikakati ya kutatua hali hiyo.
Akizungumza katika eneo la Athi River kwenye hafla ya Uzinduzi wa ujenzi wa nyumba elfu 15 chini ya mpango wa Serikali wa ujenzi wa makaazi ya gharama nafuu, Macharia amesema kwamba Shirika la Kitaifa la ujenzi limepiga hatua kubwa katika kufanikisha agenda za Rais Uhuru Kenyatta katika Serikali ya Jubilee.
Macharia aidha ametaka Shirika hilo kujitahidi kufanikisha mpango wa Serikali wa kuwapa Wakenya nyumba za gharama ya chini akisema kwamba Wiziara yake itafanya kila juhudi kufanikisha mradi huo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu katika Wizara ya Ujenzi Charles Hinga pamoja na Mbunge wa Mavoko Patrick Makau.