HabariNewsSiasa

Hafla ya kuchangisha fedha za kufadhili kampeni za Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga imehairishwa.

Hafla ya kuchangisha fedha za kufadhili kampeni za Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga imehairishwa hadi siku isyojulikana.
Uchangishaji huo ambao ulipewa Raila’s One Million Shillings Campaign Dinner, uliratibiwa kufanyika siku ya Jumanne wiki ijayo.
Licha ya kukosa kutaja sababu kuu za kuhairisha kikao hicho, ofisi ya Raila chini ya Azimio la Umoja imesema kwamba itatangaza siku nyengine ya hafla hiyo.
Hata hivyo, ofisi ya Odinga imesisitiza kwamba siku ya Ijumaa wiki ijayo, itafanya Kongamano la Kitaifa la Azimio la Umoja japo haijatangaza eneo la kikao hicho.