HabariNews

Wakenya wawili waliowasilisha ombi kwa Tume ya Mahakama ya JSC wakitaka Jaji Saidi Chitembwe aondelewe ofisini wameliondoa ombi hilo.

Wakenya wawili waliowasilisha ombi kwa Tume ya Mahakama ya JSC wakitaka Jaji Saidi Chitembwe aondelewe ofisini wameliondoa ombi hilo.
John Wangai na Stephen Ooko ambao waleiondoa ombi hilo mapema hii leo, wamesema kwamba halijashughulikiwa kulingana na sharia huku wakidai kwamba wamechukua hatua hiyo kwa kuwa walihisi kwamba huenda sharia isifatwe katika Tuhuma walizowasilisha dhidi ya Chitembwe.
Hata hivyo kuna maombi mawili dhidi ya Jaji Chitembwe ambayo yangali mbele ya JSC huku vikao vya kuyasikiliza vikiratibiwa kuanza rasmi Disemba 14.
Itakumbukwa kwamba aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi Mike Sonko ni miongoni mwa walioagizwa kufika mbele ya JSC kutoa mwanga Zaidi kuhusu madai aliyoibua kuhusu Jaji Chitembwe kabla ya vikao hivyo kuanza.
Hii sio mara ya kwanza kwa madai ya ufisadi kumuandama Jaji huyo, Julai mwaka huu alikamatwa pamoja na Aggry Muchelule kisha kuwasilishwa katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi DCI ambapo alirekodi taarifa kufuatia madai kwamba wlikuwa wanapanga kupokea hongo.