HabariNews

WATU 3 ZAIDI WAOKOLEWA KUTOKA KWENYE MGODI ULIOPOROMOKA BONDO KAUNTI YA KISUMU.

Watu watatu zaidi wameokolewa wakiwa hai kutoka mgodi ulio poromoka mapema mwezi huu ,eneo la Bondo kaunti ya Kisumu ambapo kufikia sasa watu 6 wameokolewa.
Kulingana na naibu wa kamishina eneo hilo,Richard Karani,watatu hao waliokolewa mapema hii leo na kwasasa wamepelekwa katika hospitali ya Bondo ambapo wanaendelea kupokea matibabu.
Kamishina huyo ameongeza kwamba mwili wa mtu 1 umepatikana akiongeza kuwa kumesalia mtu mmoja ambaye amesalia ndani ya mgodi huo kwa siku ya saba sasa.
Aidha juhudi za muokoa mwathiriwa huyo zingali zinaendelea.

BY NEWSDESK