HabariNewsSiasa

IEBC YASEMA HAINA UWEZO WA KUWAZUIA WANASIASA KUENDELEZA KAMPENI ZAO ZA MAPEMA.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inasema kwamba haina uwezo wa kisheria kuwazuia wanasiasa wanaoendeleza kampeni za mapema zinazoendelea kushuhudiwa humu nchini.
Akizungumza juu ya suala hilo, mwenyekiti wa tum hiyo Wafula Chebukati anasema kwamba tume hiyo inauwezo wa kudhibiti kampeni miezi mita kabla ya uchaguzi mkuu kulingana na katiba.
Hata hivyo , Chebukati anakiri kuwa wanasiasa wanavunja sheria kwa kufanya kampeni zao mapema na hivyo anatoa wito kwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Uma,DPP kuwachukulia hatua wanasiasa wote wanaovunja sheria kwani afisi yake haina uwezo wa kisheria kufanya hivyo.

BY NEWSDESK