HabariNews

VIJANA WASHAURIWA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUSHIRIKIANA NA IDARA ZA USALAMA KUDUMISHA AMANI

Mashirika yasioyakiserikali ukanda wa pwani yameshauri kina mama pamoja vijana kushirikiana na maafisa wa polisi katika kuhakikisha uwepo wa usalama na amani miongoni mwa jamii .

Akizungumza kwenye kongamano la amani na usalama katika hoteli moja mjini mombasa Evans Kasena, ambae ni msimamizi wa vijana katika mashirika yasiokiserikali amewahimiza jamii hasa kina mama pamoja na vijana kushirikiana idara ya usalama ili kujenga amani hasa msimu huu wa kisiasa.
Wakati huo huo Kasena amewasihi jamii kuwa wenye kutoa taarifa wanapohisi kwamba kuna dalili za kudorora kwa usalama hasa wakati huu ambapo baadhi ya wanasiasa wanaonekana kutumia vibaya vijana na kina kuzua vurugu kwenye minuting za kisiasa.
kongomano hilo lilimewaleta pamoja maafisa wa usalama mashirika yasiokiserikali pamoja na wasomi .

BY NEWSDESK