HabariNews

WAKENYA KUSUBIRI KWA HAMU KUNUFAIKA NA GHARAMA YA CHINI YA UMEME.

Gharama ya umeme humu Nchini inatarajiwa kushuka kwa asilimia 15 kuanzia Mwezi huu wa Disemba.
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza hayo kwenya sherehe za mwaka huu za Jamuhuri ambapo amesema kwamba gharama hiyo itapungua kwa jumla ya asilimia 30 huku asilimia 15 nyengine ya kupunguzwa kwa gharama, itafanyika mapema mwaka ujao.
Tangazo hilo la Rais aidha, linanuia kuwapa afueni Wakenya ambao wamekuwa wakilalamikia kupanda maradufu kwa gharama ya umeme humu Nchini.

BY NEWSDESK