HabariLifestyleSiasa

Ukosefu wa Demokrasia umetajwa kuchangia kuendelea kubuniwa kwa vyama Zaidi vya kisiasa humu Nchini.

Ukosefu wa Demokrasia umetajwa kuchangia kuendelea kubuniwa kwa vyama Zaidi vya kisiasa humu Nchini.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Chama cha hivi punde Zaidi cha kisiasa humu Nchini cha DAP-KENYA, viongozi ambao walijuhusisha na Chama cha FORD KENYA, wameendelea kuushtumu uongozi wa Chama hicho kwa kusababisha waliokuwa wanachama kujiondoa na kubuni Chama kipya.
Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa amesikitishwa na Chama cha FORD KENYA kutoafikia matarajio ya kukuza demokrasia licha ya kuwa miongoni mwa vyama vya kwanza kabisa kubuniwa baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi humu Nchini.
Kauli sawa na hiyo ilitolewa na aliyeku kiongozi wa mrengo hasimu wa Ford Kenya Wafula Wamumnyinyi ambaye kwa sasa ndie kiongozi wa chama hicho cha DAP-K .
Ikumbukwe kwamba chama cha Ford kilianziishwa rasmi mwaka wa 1991 na viongozi sita ambao ni Jaramogi Oginga Odinga, Philiph Gashoka, Ahmed Bahamaris, Salim Ndamwe, Masinde Muliro na John Tenge.
Hata hivyo kufikia mwaka 1962 chama hicho kilivunjika na kuwa Ford Kenya na Ford Asili vikiongozwa na Jaramogi Oginga Odinga na Keneth Matiba mtawalia.

BY NEWSDESK