HabariNewsSiasa

HAKUNA YEYOTE ATAKAYEIBA KURA ZANGU MWAKA HUU WA UCHAGUZI MKUU ASEMA NAIBU WA RAIS.

Naibu wa Rais William Ruto yuko katika Kaunti ya Trans Nzoia kuendelea na kampeni zake za kuwarai wakaazi kumpigia kura wakati wa Uchaguzi wa Agosti 9.
Ruto amewahakikishia wakaazi wa Trans Nzoia na Kenya kwa jumla ya kwamba hakuna yeyote atakayeiba kura zake mwaka huu wa uchaguzi mkuu.
Kwenye hotuba yake kwa halaiki ya wananchi katika eneo la Kachobora, Naibu wa Rais ametoa wito kwa Wakenya kutokubali kuingizwa woga wa Deep state na vitengo vyengine vya serikali kuzima ndoto yake.
Wakati uo huo RUTO, amesisitiza kwamba yuko tayari kukamilisha miradi waliokuwa wameanzisha na Rais Uhuru Kenyatta iwapo ataibuka kuwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wkati uo huo Ruto ameemdeleza shutuma zake dhidi ya Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga akidai kwamba, ndiye aliyelemaza mipango ya kuwatimizia Wakenya ahadi walizotoa.
Ikumbukwe kwamba Ruto, ameandamana na Wabunge kadhaa akiwemo Dan Wanyama, Didmus Barasa wa Kimilili, Caleb Kositany wa Soy, aliyekuwa Mbunge wa Cherengany Wesley Korir, John Waluke wa Sirisia miongoni mwa wengine.

BY NEWSDESK