HabariNewsSiasa

MAHAKAMA KUTATUA MZOZO WA KIWANGO CHA FEDHA ZINAZOTUMIWA NA VYAMA VYA KISIASA…

Mvutano kuhusu kiwango cha fedha kinachostahili kutumiwa na vyama vya kisiasa na wanasiasa wanaolenga nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu sasa umeelekea mahakamani.
Mashirika mawili ya kijamii yamewasilisha kesi dhidi ya tume ya uchaguzi IEBC na bunge la kitaifa kufwatia hatua ya kubatilishwa kwa agizo la awali la kudhibiti kiwango cha fedha kinachostahili kutumika katika kampeni.
Katika kesi hiyo mashirika ya katiba institute na Afrikogyamelishtumu bunge la kitaifa kwa kufanya uamuzi kinyume na katiba na kubatilisha notisi iliyochapishwa agosti mwaka uliopita na IEBC kuhusu mwongozo wa kiwango cha fedha kinachostahili kutmika katika kampeni hatua iliyofanya tume hiyo kufutilia mbali notisi hiyo.
Hatua hiyo ilimaanisha kwamba sasa vyama vya kisiasa na wanasiasa vile vile walikua na uhuru wa kutumia jinsi wanavyotaka fedha katika kampeni na haingewalazimu kuweka wazi matumizi yao.
Hata hivyo uamuzi huo uko mikononi mwa mahakama ikiwa ni miezi saba tu kabla uchaguzi mkuu.
Katika notisi iliyochapishwa awali wawaniaji wa urais walihitajika kutumia sh bilioni 4.4 katika kampeni huku watu ambao wangetaka kutoa ufadhili kwa wawaniaji wakitakiwa kutoa asili mia 20 tu ya fedha hizo ambazo ni sh milioni 830.
Vyama vya kisiasa vingeruhusiwa kutumia sh milioni 17.7. aidha wawaniaji wa ugavana wangeruhusiwa kutumia sh milioni 21.9 na wanaolenga nyadhifa ya wawakilishi wa kike wangetumia sh milioni 21.9 kwa kuzingatia idadi ya watu na ukubwa wa eneo.
Ikumbukwe bunge lilipinga agizo hilo la IEBC likisema kwamba lilichapishwa baada ya mda unaohitajika kisheria kukamilika yaani miezi 12 kabla ya uchaguzi mkuu.

BY NEWSDESK