HabariLifestyleNews

POLISI HUKO KWALE WAMSAKA MWANAMUME ANAYEDAIWA KUWAUWA KWA KUWACHINJA WANAWE WAWILI.

Polisi katika eneo la Kinango katika Kaunti ya Kwale wanamsaka mwanamume aliyewaua wanawe wawili kwa kuwakata shingo siku ya Jumapili.
Kulingana na kamanda wa polisi wa kinango Fredrick Ombaka, ni kwamba mshukiwa huyo kwa jina la Charlse Maingi Mutie, umri 54 aliwakata shingo wanawe Perilian Nduki mwenye umri wa miaka 5 na Maratina Maingi mwenye umri wa miaka 7 mmoja baada ya mwengine.
Inaarifiwa kwamba Mutie, aliwafanyia unyama huo wanawe kufuatia mzozo baina yake na mkewe kwa jina Bretin Ndung’i Mwema, ambaye alitoroka baada ya kugunduwa maisha yake yalikuwa hatarini.
Miili ya Maratina na Perilian aidha, imehifadhiwa katika hospitali ya Kinango ambako itafanyiwa upasuaji.

BY EDITORIALDESK