HabariNews

MTU MMOJA AMEUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KATIKA KIJIJI CHA BOBO WADI YA HINDI KAUNTI YA LAMU.

Mtu mmoja ameuawa kwa kuchomwa moto katika kijiji cha Bobo wadi ya Hindi kaunti ya Lamu.
Mwenyekiti wa kitaifa wa Tume ya uajiri wa polisi NPSC Eliud Kinuthia amesema mauaji hayo yanafanana na yale ya jana katika eneo la Widho-Majembeni, ambapo watu sita waliuawa kwani marehemu alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma kabla ya kuteketezwa.
Amesema mbali na kuuawa kwa jamaa huyo kwa jina John Monji nyumba pamoja na mali yake pia vimeweza kuteketezwa.
Aidha amewapongeza maafisa wa usalama kwa kufika katika eneo la mkasa kwa haraka na kuzuia maafa zaidi.

BY EDITORIAL DESK.