HabariKimataifaNews

Burundi yawafukuza Wanyarwanda 12 kwa kukataa chanjo ya Covid.

Wanyarwanda 12 wakiwemo wanawake na watoto wamefukuzwa na mamlaka ya Burundi baada ya kukataa kupata chanjo ya Covid.
Raia hao wa Rwanda walikaa zaidi ya siku tano katika eneo la Nyakarama hill katika jimbo la Kirundo kaskazini mwa Burundi.
Walisema wamekimbia kampeni ya lazima ya chanjo inayoendelea nchini Rwanda.
Gavana wa jimbo la Albert Hatungimana aliagiza warudishwe Rwanda.
Alhamisi iliyopita, raia wengine tisa wa Rwanda walirejeshwa nchini kwao na mamlaka ya Burundi katika jimbo hilo.
Pia walikuwa wamekimbia kampeni ya lazima ya chanjo.

BY EDITORIAL DESK