HabariKimataifaNews

Zoezi la kuwaokoa watu walioripotiwa baada ya boti kuzama kisiwani Pemba limesitishwa.

Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi wa timu ya kikosi cha wapiga mbizi KMKM Kasim Khalfan kuthibitisha kuwa taarifa za sasa hazioneshi ushahidi wa watu waliopotea majini.
Usiku wa kwanza miili kumi ilipatikana na watu kumi waliokolewa.
Hata hivyo siku ya pili timu ya uokoaji haikumpata mtu mwingine yeyote.
Mamlaka za eneo hilo ziliulizwa kuripoti ikiwa kuna watu wengine zaidi waliopotea na hakuna yeyote mpaka sasa.

BY EDITORIAL DESK