HabariNews

Idara ya kitaifa ya huduma kwa vijana nys yatangaza nafasi za usajili wa vijana katika idara hiyo.

Idara ya kitaifa ya huduma kwa vijana nys imetangaza nafasi za usajili wa vijana katika idara hiyo unaotarajiwa kuanza wiki ijayo jumatatu tarehe 10 mwezi huu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kulingana na taarifa kutoka kwa idara hiyo, usajili huo unatarajiwa kuanza mwendo wa saa mbili asubuhi katika maeneo bunge mbalimbali huku mkoani pwani ikiwa zamu ya maeneo Bunge ya nyali, kinango, lamu mashariki, kilifi kusini, tana kaskazini na rabai.
Hata hivyo, ili kupata nafasi katika idara hiyo ni lazima uwe na kiwango cha gredi ya D kuenda juu, uwe mwenyeji wa eneo bunge husika, uwe na umrii wa baina ya miaka 18-24 miongoni mwa mengine.

BY EDITORIAL DESK