HabariNews

Kamishna wa Kwale Gideon Oyagi awataka wavuvi eneo la shimoni kuzingatia sheria za uvuvi.

Kamishna wa kaunti ya Kwale Gidion Oyagi amewataka wavivi eneo la shimoni kuzingatia sheria za uvuvi zilizowekwa na serikali.
Akizungumza mjini Kwale Oyagi amewataka wavuvi kufanya kazi ndani ya sheria zilizowekwa na serikali na kuwahakikishia wavuvi hao kwamba ofisi yake itahakikisha hawahangaishwi na maafisa wa polisi.
Kauli hii inajiri kufuatia malalamishi ya kukamatwa kwa wavuvi na maafisa wa polisi hali inayoathiri shughuli zao za uvuvi ambazo ndizo tegemeo lao kuu.

BY EDITORIAL DESK