HabariNews

SERIKALI KUANZA TENA ZOEZI LA KUWAPA WAZEE RUZUKU YA KILA MWEZI YA INUA JAMII.

Ni afueni kwa Wakongwe na walemavu humu nchini baada ya serikali ya kitaifa kuwahakikishia kuwa watapata ruzuku yao ya kila mwezi ambayo imecheleweshwa kwa takriban miezi sita sasa.
Kulingana na takwimu, Wakenya zaidi ya milioni moja ambao pia wanajumuisha mayatima, hawajapata ruzuku hiyo tangu julai mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa serikali, kwa sasa wote watalipwa kulingana na malimbikizi ya mwezi julai na oktoba kwa kuzingatia bajeti ilioko.