HabariNewsSiasa

Naibu wa Rais William Ruto anatarajiwa kuzuru maeneo kadhaa katika Kaunti ya Machakos hii leo kuendeleza kampeni zake za kuwania Urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Naibu wa Rais William Ruto anatarajiwa kuzuru maeneo kadhaa katika Kaunti ya Machakos hii leo kuendeleza kampeni zake za kuwania Urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.
Ruto aidha anatarajiwa kuhutubiwa mikutano ya hadhara katika maeneo ya Donyosabok na Tala katika eneo bunge la Matungulu mapema leo asubuhi kisha baadae kuendeleza misururu ya mikutano katika maeneo ya Kangundo, Kakuyuni na Kidhaani katika eneo Bunge la Kangundo.
Swali ni je Ziara ya Naibu wa Rais William Ruto Ukambani itafaulu kumshawishi Kiongozi wa WIPER Kalonzo Musyoka kujiunga naye kwenye kinyang’anyiro cha Urais?
Itakumbukwa kwamba ziara ya Ruto inajiri siku nne tu baada ya Kalonzo kutangaza kwamba hatakuwa kwenye debe kwenye wadhifa huo kwenye mkutano aliouandaa kwenye boma lake eneo la Yatta Kaunti ya Machakos.