HabariNews

Mshukiwa mkuu wa mauji ya bawabu moja katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa amekamatwa katika eneo la ufuo wa bahari.

Mshukiwa mkuu wa mauji ya bawabu moja katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa amekamatwa katika eneo la ufuo wa bahari katika bustani la Mama Ngina.
Akithibitisha kukamatwa kwake Mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI eneo la Likoni Richard Koiyer amesema Douglas Njenga mwenye umri wa miaka 20 atawasilishwa mahakamani baadaye leo.
Njenga anadaiwa kumuua Hamisi Kadida ambaye ni bawabu mwezi agosti mwaka uliopita na kisha kuutupa mwili wa marehemu kwenye kisima cha futi 40.